MWALIMU NEW VISION MIRERANI AJINYONGA SHULENI

Na Mwandishi wetu, Babati

MWALIMU wa shule binafsi ya awali na msingi New Vision ya mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, amejfariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) George Katabazi akizungumza na waandishi wa habari amemtaja mwalimu huyo kuwa ni John Msinga (34) mkazi wa kitongoji cha Songambele mji mdogo wa Mirerani.

Kamanda Katabazi amesema mwalimu Msinga amefariki dunia kwa kujinyonga akiwa ndani ya ghala la kuhiifadhi chakula cha shule hiyo.

“Mwalimu huyo alijinyonga kwenye stoo ya kuhifadhi mahindi ya shule hiyo kwa kutumia kamba aina ya manila na akadariki dunia papo hapo,” amesema.

Amesema tukio hilo lilitokea Julai 14 mwaka 2024 saa 10 jioni baada ya mwangalizi wa watoto wa shule hiyo Paulo Essau kumkuta mwili wake ukiwa umening’inia kwenye ghala hilo.

Amesema bado hawajabaini chanzo cha tukio hilo na polisi wanaendelea na uchunguzi wake na hakuna mtu wanayemshikilia juu ya kifo hicho.

Amesema mwili wa marehemu mwalimu huyo umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha kituo cha afya Mirerani.

Mkurugenzi wa shule ya New Vision, Prisca Msuya (Kio) amesema hafahamu chanzo cha kifo hicho cha mwalimu huyo kujinyonga.

Amesema mwalimu huyo alikuwa amekwenda nyumbani kwao hivi karibuni na kisha akarudi baada ya wiki moja ila akawa mkimya mno.

“Alikuwa mpweke mno kila wakati ni mkimya na akiulizwa hajibu kiitu chochote kile mara nyingi akawa amejitenga ya peke yake bila kuwa na mtu,” amesema.

Amesema ingelikuwa vyema endapo angezungumza chochote kinachomsibu ila akawa hazungumzi na ndipo walipochukua uamuzi huo.

Amesema bado wanawasubiria ndugu wa marehemu ambao ndiyo wataamua taratibu za maziko zitakapokuwa ili azikwe.

Related Posts