MWENYEKITI UWT KIBAHA MJI AWAFUNDA WANAWAKE KATA YA TUMBI NA SOFU KUCHUKUA FOMU

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Jumuiya  ya umoja wa wanawake  (UWT) Wilaya  ya Kibaha mjini imewahimiza wakinamama  kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi  kuchukua fomu bila ya uwoga wowote  kwa ajili ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi  hasusan katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa  ambao unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa UWT Elina Mgonja wakati wa ziara yake ya kikazi  katika Kata ya tumbi na Sofu yenye lengo la kuweza kuangalia uhai wa chama pamoja na kuwahimiza wanawake kushiriki  kikamilifu katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Mwenyekiti huyo aliongeza kwamba lengo lake kubwa la  kufanya ziara hiyo ni kuwatembelea wanawake katika kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini ikiwa sambamba na kuangalia mwenendo mzima wa zoezi la uandikishaji wa wanachama kujisajili  kwa mfumo wa kisasa  kwa njia  ya  kieletroniki.

“Kwa kweli nimefarijika sana nimeamua kufanya ziara yangu ya kikazi ya kutembelea  kata mbali mbali ambazo zipo katika Jimbo la Kibaha mjini na lengo lake kubwa ni kuweza kuangalia uhai wa chama jinsi ulivyo ikiwa sambamba na kuona namna ya zoezi zima la wanachama kujiandikisha kwa njia ya Kieletroniki,”alisema Mgonja.

Kadhalika aliwaomba wanawake wa Kata ya Tumbi  pamoja na kata ya Sofu kuendelea kumpa ushirikiano wa kutosha Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa sambaamba na kumuheshimisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kupiga kura kwa wingi ili kushinda kwa kishindo kikubwa na kuchukua mitaa yote bila kupoteza.

Kwa uapnde wake  Diwani wa viti maalumu Selina Wilson amewahimiza wakinamama kutorudi nyuma katika kugombea katika nafasi mbali mbali ikiwa sambamba na kuchukua fomu  kwa ajili ya kuwania nafasi mbali mbali za uongoz ikiwa sambamba na kuchangamkia fursa za mikopo zilizopo ambazo zitawasaidia katika kujikwamua kiuchumi.

Naye Diwani wa viti maalumu Shufaa Bashili amewataka wakina mama pindi wanapopata mikopo kuhakikisha kwamba wanaifanyia kazi pamoja na kuirejesha ikiwa sambamba na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Diwani wa viti maalumu wa Kibaha mjini Lidya Mgaya alisema kwamba wanawake wanapaswa wasiogope na kwamba wataendelea kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika masuala mbali mbali ya kimaendeleo.

 Mwenyekiti wa UWT Wilaya yaKibaha mjini amefanya ziara yake ya kikazi  katika kata mbili za Tumbi pamoja na kata ya Sofu ambapo ameambatana na baadhi ya madiwani wa viti maalumu pamoja na  wajumbe wa  kamati ya utekelezaji sambamba na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM. 


Related Posts