BEKI Mkenya, Joash Onyango msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi cha Dodoma Jiji baada ya usajili wake kukamilika kuichezea timu hiyo kwa mkopo wa miezi sita.
Onyango kwa mara ya kwanza kucheza Ligi Kuu Bara ilikuwa msimu wa 2020/21 ambapo alijiunga na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya na baada ya kuachana naye alijiunga na Ihefu ambayo kwa sasa inajulikana kama Singida Black Stars.
Chanzo cha ndani kutoka Dodoma kinasema usajili wake umekamilika na wakati wowote atajiunga na wenzake kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
“Onyango ni beki mzuri, kafanya kazi na kocha Mecky Maxime wakiwa Ihefu, jambo ambalo litakuwa jepesi kwake kufanya kazi zake kirahisi kukutana na kocha anayefahaniana naye,” kimesema chanzo hicho.
Chanzo hicho kimeongeza,” uwepo wa Onyango katika kikosi chetu,utaongeza kitu kikubwa kutokana na uzoefu wake pia hana papara uwanjani, hivyo tunatarajia atakuwa mfano wa kuigwa dhidi ya wenzake.”