Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Majengo ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Rukwa kilichopo Kata ya Momoka, Sumbawanga tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia nafaka ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi wa Chakula (NFRA) Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na viongozi mbalimbali, Wanafunzi na Wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Adolph Mkenda wakati akimuonesha Majengo ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga yaliyopo Kata ya Momoka tarehe 16 Julai, 2024.