RC CHALAMILA APOKEA MELIVITA YA MATIBABU KUTOKA JESHI LA CHINA ‘PEACE ARK’ – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Julai 16,2024 amepokea Melivita ya matibabu iitwayo ‘Peace Ark’ ya Jeshi la ukombozi la watu wa China katika Bandari ya Dar es Salaam.

 

RC Chalamila akizungumza wakati wa mapokezi hayo amesema Melivita hiyo itakuwepo katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za kitabibu kwa wakazi wa mkoa huo na watanzania kwa ujumla kuanzia Julai 16 hadi Julai 23, 2024.

 

Huduma hizo za kitabibu zinatolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka sitini (60) ya ushirikiano kati ya Tanzania na China na maadhimisho ya miaka sitini (60) tangu kuanzishwa kwa JWTZ mnamo Septemba 01,1964.

 

Aidha RC Chalamila amesema huduma za kitabibu zinazotarajiwa kutolewa ni pamoja na vipimo, tiba za kawaida pamoja na upasuaji wa kawaida, magonjwa ya kina mama, mifupa, njia ya mkojo, macho, pua, koo, meno, moyo, utumbo pamoja na ngozi zilizoungua na moto ambapo matibabu hayo yatatolewa kwa ushirikiano wa wataalamu wa Afya wa JWTZ, Hospitali ya Taifa Muhimbili,Tumbi, Amana, Mwananyala,Temeke na Jeshi la China.

 

Vilevile kutakuwa na kikundi cha Madaktari Bingwa watakaokuwa wanakwenda kutoa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mbagala, Hospitali ya Lugalo pamoja na Kunduchi, Hospitali ya Amana, Bunju, Mwananyamala na Temeke pamoja na maeneo mengine ambayo ratiba rasmi itatolewa na JWTZ.

 

Sanjari na hilo amesema wananchi watakaokwenda Bandarini kwenye Meli hiyo kwa ajili ya kupata matibabu wanataarifiwa wapitie geti namba mbili (2) la Bandari ya Dar es salaam.

Related Posts