TANZANIA NA OMAN ZASAINI MABORESHO YA MKATABA WA USAFIRI WA ANGA

Tanzania na Oman zimesaini maboresho ya mkataba wa Usafiri wa Anga (BASA) ambapo Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa  ameiwakilisha Tanzania kwenye utiaji saini huo na Oman imewakilishwa na rais wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi hiyo Mhandisi Ali Nabri.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali akiwemo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Biseko Chiganga, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Daniel Malanga, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Musa Mbura pamoja na maafisa kutoka nchi zote mbili.

Azma ya kufungulia masoko kwa mashirika ya ndege ya Tanzania kwenda Oman ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia ziara yake ya kikazi nchini Oman na utekelezaji wa kampeni ya Royal Tour.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Waziri Mbarawa alisema mkataba wa awali ulisainiwa mwaka 1982 hivyo maboresho yalikuwa ni muhimu, mkataba huu sasa utafungua fursa mpya za usafiri baina ya nchi mbili hizi, kuleta ongezeko la abiria pamoja na kukuza biashara na uchumi.

Kwa upande wake rais wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi hiyo Mhandisi Ali Nabri alisema hafla hiyo ni sehemu muhimu sana katika siyo tu katika kuongeza ushirikiano kati ya Tanzania na Oman bali ni hatua muhimu katika kuboresha mazingira ya biashara na kukuza uchumi wa nchi zote mbili.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na Rais wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi Oman Mhandisi Ali Nabri wakisaini mkataba wa makubaliano wa maboresho ya mkataba wa Usafiri wa Anga (BASA) uliofanyika katika ukumbi wa Watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na Rais wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi Oman Mhandisi Ali Nabri wakibadilishana mkataba wa makubaliano wa maboresho ya mkataba wa Usafiri wa Anga (BASA) uliofanyika katika ukumbi wa Watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na Rais wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa nchi Oman Mhandisi Ali Nabri wakionesha mkataba wa makubaliano wa maboresho ya mkataba wa Usafiri wa Anga (BASA) uliofanyika katika ukumbi wa Watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano wa maboresho ya mkataba wa Usafiri wa Anga (BASA) uliofanyika katika ukumbi wa Watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Related Posts