TETESI ZA USAJILI BONGO: Ambokile anasa kwa KenGold

STRAIKA aliyemaliza mkataba ndani ya kikosi cha Mbeya City inayoshiriki Ligi ya Champioship, Eliud Ambokile, yupo kwenye hatua za mwisho kujiunga na timu ya KenGold.

KenGold iliyopanda daraja kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao inaendelea kukisuka kikosi chake huku ikitua kwa Ambokile ikiwa na matumaini kwamba atakuwa msaada eneo la ushambuliaji kutokana na uzoefu alionao.

Taarifa zinaonyesha kwamba mshambuliaji huyo aliyewahi kuzitumikia kwa nyakati tofauti timu za TP Mazembe ya DR Congo na Nkana FC ya Zambia, kuna uwezekano mkubwa wa kumwaga wino ndani ya kikosi hicho ambacho msimu uliopita kiliibuka na ubingwa wa Championship.

Hadi sasa KenGold haijatangaza nyota wapya wala wachezaji ilioachana nao ikiendelea kufanya mambo kimya kimya kwa ajili ya maandalizi ujao wa mashindano.

Related Posts