Utafiti wataja dawa ya udanganyifu vyuo vikuu

Ripoti ya utafiti ya wasomi watatu, imebainisha namna vyuo vinavyoweza kukabiliana na tatizo la udanganyifu kwenye mitihani.

Mmoja wa watafiti hao, Joseph Abel ameelezea namna alivyoufanya utafiti huo na wenzake Rebecca Sima na Theresia Shavega.

Ripoti ya utafiti huo ilichapishwa kwenye jarida la European Journal of Research and Reflection in Educational Sciences Vol. 8 No. 9, 2020 ISSN 2056-5.

Watatu hao walitoa ripoti hiyo kuhusu udanganyifu unaofanywa na wanafunzi vyuoni waliouita kwa jina la: ‘The intensity of academic dishonesty among postgraduate students in higher learning institutions in Tanzania and how to curb the situation,’ walishauri hatua kadhaa zinazopaswa kuchukuliwa na vyuo vikuu.

“Vyuo vya elimu ya juu vinatazamwa kama chanzo cha ukweli na uaminifu ambapo wanafunzi wanaundwa katika nyanja zote za kitaaluma na maadili,” anasema Abel alipoongea na gazeti hili.

Anasema utafiti wao ulijumuisha wanafunzi wa shahada ya uzamili katika kozi za elimu na sayansi ya jamii kutoka kwenye vyuo vikuu vinne nchini pamoja na maofisa wa uhakiki ubora na wakuu wa idara.

Kwa mujibu wa utafiti, kihistoria, wanafunzi katika taasisi za elimu ya juu wamekuwa wakijihusisha na udanganyifu wa kitaaluma kwa kutumia mbinu za kisasa na za kitamaduni za kudanganya kitaaluma.

Utafiti umebaini aina nyingi za udanganyifu ikiwamo kuiba taarifa za kitaaluma za wengine, nukuu au takwimu za wengine kwa mwanafunzi kufanya marejeo bila kutaja chanzo au kutoa dai la uwongo la jinsi taarifa za utafiti wake zilivyokusanywa.

Hii inahusisha mwanafunzi kuangalia kazi ya mwanafunzi mwingine wakati wa kufanya utafiti au kujaribu kuwasiliana na wengine ili kupata msaada wakati wa mtihani.

 Aina nyingine ya ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma ni wizi, ambao ni uwasilishaji wa kukusudia au bila kukusudia wa maneno ya mtu mwingine au mawazo bila uthibitisho wa wazi na sahihi.

Utafiti uliundwa ili kubainisha ukubwa wa ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma miongoni mwa wahitimu wanafunzi katika vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania na jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo.

Takwimu zilikusanywa kwa kuzingatia majadiliano ya vikundi na mahojiano. Mbinu ya ubora ilichaguliwa ili kupata uelewa wa hisia na uzoefu wa wanafunzi waliohitimu, mkuu wa idara na maofisa wa uhakiki wa ubora kuhusu ukubwa wa ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma katika taasisi za elimu ya juu na jinsi tatizo hilo linavyoweza kumalizwa.

Majadiliano ya kikundi yalichaguliwa kama zana ya kukusanya takwimu kwa sababu katika baadhi ya matukio, mijadala hii ilizalisha fikra mpya miongoni mwa washiriki jambo ambalo lilisababisha mjadala wa kina zaidi.

Takwimu zilikusanywa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Iringa. Haya maeneo yalichaguliwa kimakusudi kwa sababu yana idadi kubwa ya vyuo vikuu vinavyotoa programu mbalimbali za shahada.

Washiriki walitolewa kutoka vyuo vikuu vinne vinavyotoa programu za sayansi ya jamii. Jumla ya vikundi nane vilishiriki majadiliano yaliyofanyika katika vyuo vikuu vinne. Kila kundi lilikuwa na washiriki kumi. Pia, jumla ya wakuu wa idara wanane na maofisa uhakiki ubora wanane walihojiwa.

Washiriki wa utafiti huo walijumuishwa wanafunzi wa shahada ya uzamili katika kozi kadhaa zikiwamo za elimu na sayansi ya jamii kutoka vyuo vikuu vine. Pia utafiti uliwajumuisha maofisa wa uhakiki ubora wa elimu na wakuu wa idara.

 Data zilikusanywa kupitia majadiliano ya vikundi na mahojiano. Matokeo ya utafiti yameonyesha suala la uadilifu wa kitaaluma unaweza kulindwa katika taasisi za elimu ya juu kwa njia mbalimbali.

Utafiti huo unabainisha mambo kadhaa ambayo yakitekelezwa yanaweza kupunguza tatizo la udangayifu wa mitihani vyuoni.

Kozi ya maadili muhimu vyuoni

Miongoni mwa mambo hayo ni taasisi za elimu ya juu kuanzisha kozi ya maadili ya kitaaluma.

“Kozi ya maadili ya kitaaluma itasaidia mwanafunzi kuelewa masuala mbalimbali kuhusu uadilifu kitaaluma na jinsi ya kuudumisha. Na kupitia tathmini zinazotolewa mwishoni mwa muhula, mhadhiri atapata maoni juu ya kiwango cha uelewa wa wanafunzi wa kozi kwa hakika,” inasema sehemu ya ripoti ya utafiti huo.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kuanzisha kozi ya maadili ni muhimu kwa kuwa itawawezesha wahadhiri kufuatilia mienendo ya wanafunzi hasa inayohusiana na udanganyifu wa kitaaluma.

Pia, mhadhiri ataweza kujadiliana na wanafunzi wanaodanganya kuhusu jinsi ya kudumisha uadilifu kitaaluma.

Utafiti huo pia ulionyesha kuwa suluhisho lingine, ni wahadhiri na wanafunzi kufanya mijadala juu ya namna wanavyoweza kudumisha taaluma na uadilifu.

“Ilishauriwa kuwa wahadhiri wanapaswa kutumia dakika chache wakati wa saa za kufundisha kujadili masuala kuhusu ukosefu wa uaminifu kitaaluma. Madarasa yale ambayo wahadhiri huchukua muda kujadili kuhusu ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma, yana matukio machache sana ya wanafunzi kufanya udanganyifu wa kitaaluma,” inasema ripoti.

Matumizi ya programu maalum za kiteknolojia

Pia, utafiti huo ulishauri matumizi ya programu maalum za kisasa za kugundua wizi wa kitaaluma, hali itakayowafanya wanafunzi kuheshimu vyanzo ambavyo wamevitumia katika kazi zao ili kuepuka wizi kitaaluma.

“Ikiwa wahadhiri watatumia programu ya kugundua wizi, wataweza kuona kazi ambayo imeibwa na kuwaadhibu wanafunzi kulingana na sheria na kanuni ambazo chuo kikuu kimeweka,” inaeleza.

Kubadili muundo wa upimaji

Kwa mujibu wa utafiti huo, wahadhiri wanapaswa kubadili mbinu zao za sasa za upimaji na kuweka uzito kwenye upimaji wa kuzungumza ana kwa ana badala ya kuandika zaidi.

“Ni wakati wa semina na mawasilisho ya nadharia ambapo tunaweza kutambua kwa urahisi wanafunzi wasio waaminifu. Wengi wao hushindwa kujibu maswali yaliyoulizwa na wanajopo.

“Wanakubali kila maoni bila kutoa ufafanuzi wowote. Ikiwa tungekuwa wakali sana kwa hili wengi wao wangefeli,” utafiti ulinukuu mahojiano na mkuu wa idara ya chuo kikuu kimoja.

Mkuu wa idara wa chuo kikuu kingine kwenye utafiti huo alinukuliwa akisema: “Wakati wa mawasilisho ya semina au tasnifu, ni rahisi sana kutambua wanafunzi wasio waaminifu kwa kuwa hukosa imani katika kujibu maswali kutoka kwa wanajopo.

“Baadhi yao hawawezi kujibu swali lolote; wanakaa kimya tu baada ya kumaliza mawasilisho yao.”

Pia, ilipendekezwa vyuo viwe vinaalika watahini wa nje pale wanafunzi wanapomaliza kuwasilisha tasnifu na nadharia zao.Watahini hawa nao wana nafasi ya kupima uwezo wa mwanafunzi na kama ana sifa ya kutunukiwa shahada.

Aidha, utafiti huo ulipendekeza vyuo vikuu kuimarisha mfumo wa kuhakikisha ubora wa ndani kwa kutoa vifaa vyote vinavyohitajika.

Matokeo ya utafiti pia yalibaini kuwa moja ya mikakati ya kudumisha uadilifu wa kitaaluma katika taasisi za elimu ya juu, ni kuwezesha vyuo vikuu kuendesha semina za mara kwa mara kuhusu majukumu ya usimamizi miongoni mwa wahadhiri ili kuhakikisha maendeleo ya kitaaluma kwa wafanyakazi yanayohusiana na uadilifu kitaaluma.

Ripoti hiyo ya utafiti ilibaini kuwa semina zitawawezesha wahadhiri kuelewa aina mbalimbali mpya za udanganyifu wa kitaaluma, ambazo wanafunzi hutumia kila wakati kwa sababu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Pia, utafiti huu umependekeza kudumisha uadilifu wa kitaaluma katika taasisi za elimu ya juu, jambo linalopaswa kutekelezwa kwa ushirikiano wa wadau wa elimu.

Utafiti unaonyesha kuwa ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma umekuwa ukifanyika katika taasisi za kitaaluma kote duniani.

Utafiti umeonyesha ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma katika elimu ya juu ni mwendelezo wa tabia hiyo kutoka shule za msingi, hasa katika wizi wa mitihani ambao unahusisha jamii na shule.

‘’Ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma unadhoofisha mojawapo ya majukumu muhimu ya taasisi za elimu ya juu, ambayo ni kuweka mazingira mazuri ya kujifunza ambayo yatazalisha wahitimu ambao sio tu wenye ujuzi wa hali ya juu na uwezo wa kiufundi, lakini pia kuonyesha viwango vya juu vya uaminifu, uwajibikaji wa kimaadili na kujitolea katika kutumikia taaluma na jamii yao vizuri,’’ inasema ripoti.

Utafiti uliofanywa nchini Zimbabwe na Chireshe (2014) kuhusu ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma, ulionyesha kuwa iliwezekana kwa wahadhiri wa vyuo vikuu kuzuia ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Hilo lilifanyika kwa vyuo kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kutaja vyanzo vya utafiti wao, kuboresha utoaji wa vifaa vya kusomea, kuboresha njia za ufundishaji, kuweka uangalizi mkali na kuhimizwa kusoma kwa bidii mfululizo.

Utafiti mwingine ambao ulifanywa Kusini Afrika na Thomas na De Bruin (2012), ulipendekeza vyuo vikuu kuwa makini katika kuanzisha utaratibu wa kushirikiana pamoja na miundo inayofungamanisha mifumo itakayoshughulikia vitendo vya udanganyifu kwa uadilifu wa kitaaluma.

Aidha, kulikuwa na utafiti uliofanywa na Omonijo, Oludayo, Uche na Rotimi (2014) kuhusu kupunguza uaminifu wa kitaaluma kwa kutumia wafanyakazi wa masuala ya wanafunzi nchini Nigeria.

Utafiti uligundua kuwa ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma unaweza kuondolewa kwa kuandaa semina za kudumisha kitaaluma uadilifu katika vyuo vikuu.

Semina kama hizo husaidia kuwakumbusha wanafunzi na wasimamizi kuhusu majukumu yao ya kudumisha uadilifu kitaaluma.

Nchini Malawi, kulikuwa na utafiti na Seleman, Chawinga na Dube (2018) kuhusu sababu za wanafunzi wa shahada ya uzamili kuiba kazi za wengine.

Utafiti huo ulipendekeza vyuo vikuu kuanzisha mafunzo ya ustadi wa juu wa uandishi wa kitaaluma kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Nchini Zambia, utafiti uliofanywa na Akakandelwa, Jain na Wamundila (2015), ulipendekeza vyuo kuanzisha sera na kanuni thabiti zinazozingatia ujio wa teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano na kujifunza njia tofauti zinazopitishwa na chuo husika.

Kwa ujumla, ukosefu wa uaminifu wa kitaaluma katika taasisi za elimu ya juu ni janga. Hata hivyo, taasisi za elimu ya juu zimekuwa zikifanya kazi kwa bidii kuondoa tatizo hili.

Taasisi za elimu ya juu zinahimizwa kuunda mikakati ya a pamoja ili kupambana na tatizo hilo.

Related Posts