Utulivu Experience yaandaa Matembezi jijini Dar es Salaam

 

Katibu wa Utulivu Experience Dkt.Mboni Kibelloh akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Matembezi na Tamasha jijini Dar es Salaam.

Afisa Sanaa Mwandamizi wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Abel Ndaga  akizungumza kuhusiana na Ushirikiano kati Utulivu Experience na Serikali jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja ya Utulivu Experience mara baada ya kuzungumza  na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

*Wasanii mbalimbali kutumbwiza ni Julai 20 mwaka huu.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
UTULIVU Experience imeandaa matembezi kwa ajili ya kuenzi viongozi mbalimbali pamoja na kuthamini Amani iliyopo nchini.
Mgeni rasmi katika Matembezi hayo ni Waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo na viongozi wengine watakuwepo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Katibu wa Utulivu Experience Dkt.Mboni Kibelloh amesema kuwa katika Matembezi hayo ni kwa ajili ya kujiandaa na Tamasha litakalofanyika Septemba mwaka huu ambapo matembezi hayo ni bure kushiriki.
Kibelloh amesema kuwa matembezi hayo yataanzia Viwanja vya Farasi Oasterbay na kuishia Aga Khani na kurudi katika Viwanja vya hivyo.
Amesema kuwa katika Matembezi hayo kwenye viwanja kutakuwa burdani za kutosha kutoka kwa wasanii akiwemo Sholo Mwamba.
Dkt.Kibelloh amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa burdani za muziki watoto nao hawajaachwa nyuma kuwepo burdani zao yakiwemo mabembea na Michezo mingine.
Hata hivyo amesema kuwa kuwa katika Matembezi hayo wenye kuleta vinywaji,Chakula pamoja vitu vya sanaa kuwasiliana na Utulivu Experience.
Amesema kuwa Utulivu Experience itaendelea kufanya vitu mbalimbali katika kuchochea Amani pamoja na kuenzi michango ya viongozi mbalimbali.
Matembezi na Tamasha hilo wanashurikiana na Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo.
Nae Afisa Sanaa Mwandamizi wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA)Abel Ndaga amesema kuna ushirikiano kati ya Utulivu Experience na Serikali
Amesema Tamasha hilo litakuwa na vitu pekee kwa viongozi mbalimbali kushiriki na kupata mawazo kwa kizazi kilichopo katika kuenzi na kuthamini Amani iliyotukuka nchini.

Related Posts