AWESU ALI AWESU NI MNYAMA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuinasa saini ya Kiungo mshambuliaji Awesu Ali Awesu kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili.

Awesu amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na KMC aliyodumu nayo kwa miaka mitatu.

Awesu ni mchezaji mzoefu kwenye Ligi Kuu ya NBC na anaweza kumudu nafasi ya kiungo wa ushambuliaji na winga zote ingawa pia amewahi kutumika kama kiungo mkabaji.

Mbali na KMC, Awesu amewahi kutimikia timu za Kagera Sugar, Azam FC na Mwadui FC kwa nyakati tofauti.

#KonceptTvUpdatesImage

Related Posts