Katibu wa NEC, itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) CPA. Amos Gabriel Makalla leo Julai 17, 2024 amekagua uwanja wa Mpira wa Miguu unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, unaotumika na Klabu ya KMC inayoshiriki Ligi kuu ya Tanzania Bara.
CPA. Makalla ambae pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, amekagua Uwanja huo, ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake yenye lengo la kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya Mwaka 2020/2025.