Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH,) Prof. Mohamed Janabi amesema matumizi ya dawa za kulevya huathiri mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha vifo vya ghafla.
Janabi amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili inahudumia watu 3840 waliothirika na dawa za kulevya ambapo kwa siku watu 900 wanaenda kunywa dawa tiba ya Methadone.
Ametoa elimu hiyo leo katika ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA,) jijini Dar es salaam ambapo pia alikabidhiwa tuzo kwa niaba ya MNH kwa jitihada zao za kupambana dhidi ya dawa za kulevya.