Serikali yaendelea na Majadiliano na Wadau na Kampuni za Uzalishaji wa Nishati Safi ya Kupikia ili Kupunguza ya gharama za Ununuzi kwa Wananchi

Serikali imesema inaendelea na majadiliano na wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za uzalishaji wa nishati safi ya kupikia ili kupunguza ya gharama za ununuzi wa bidhaa hiyo kwa wananchi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema hayo katika tamasha la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia lililoandaliwa na Taasisi ya Upskill Tanzania jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imekusudia kupunguza gharama za vifaa ili kuhakikisha kila mwananchi bila kujali kipato chake anamudu gharama za nishati safi ya kupikia ambayo ni muhimu na ya lazima kwa kila binadamu.
Mhe. Khamis amesema umaskini mkubwa katika Bara la Afrika, ni wa wanawake kutokana na kutumia muda mrefu kutafuta nishati isiyo safi ya kupikia itokanayo na kuni nyuma badala ya kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kiuchumi.
Ameongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali ya Awamu ya Sita inafanya juhudi mbalimbali za kuhamasisha wananchi kutumia nishati ya umeme, gesi na mkaa mbadala ili kuepukana na ukataji wa miti kwa ajili ya kupikia.
#KonceptTvUpdates

Related Posts