Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amewahimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya nishati chafuzi inayochangia uharibifu wa mazingira.
Amesema hayo wakati akizindua Kongamano la ‘Samia Nishati Safi Festival’ kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ni rafiki kwa Mazingira na afya ya viumbe hai.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kongamano hilo Bi. Mndeme amesema nishati safi ikiwemo matumizi ya umeme, gesi na joto la ardhi ni nyenzo kuu kwa taifa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Pia, amewaasa wananchi kuacha matumizi ya nishati chafuzi kama mkaa na kuni ambazo zinaharibu mazingira, kusababisha magonjwa ya upumuaji, vifo na athari nyingine za kijamii.
Naibu Katibu Mkuu Mndeme ameongeza kuwa nishati safi ya kupikia ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi huku akisema nishati chafuzi kama kuni na mkaa zinasababisha uharibifu wa mazingira, vifo kwa watoto wachanga, magonjwa ya upumuaji na changamoto katika familia kama ndoa kuvunjika.
#KonceptTvUpdates