JAFO: TUTAHAKIKISHA TUNATATUA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA MIPAKANI

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizungumza Leo Julai 18, 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama kuwasalimia wananchi wa mji wa Tunduma Mkoani Songwe alipopita akitoka katika ziara yake Mkoa wa Rukwa

……

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema kuwa Wizara yake itahakikisha inatatua changamoto za kibiashara katika maeneo ya mipakani ili sekta ya viwanda na biashara iweze kukua

Dkt. Jafo amesema hayo Julai 18, 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama kuwasalimia wananchi wa mji wa Tunduma Mkoani Songwe alipopita akitoka katika ziara yake Mkoa wa Rukwa

Amesema kuwa Wizara hiyo itahakikisha inatakeleza maagizo yaliyotolewa na utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema katika ziara ya Kitaifa nchini humo Oktoba 23 – 25, 2023 yanayohusu utatuzi wa changamoto za biashara katika mpaka wa Tunduma.

Aidha, Jafo amebainisha kuwa kati ya changamoto 15 zilizokuwepo katika mpaka huo, changamoto nne (4) tayari zimeshafanyiwa kazi huku akiahidi kuwa changamoto zingine zinaendelea kufanyiwa kazi.

Akifafanua zaidi, Dkt. Jafo amesema kuwa changamoto ya foleni ya malori iliyokuwa inasumbua katika mpaka wa Tunduma iliyotokana na skana imetatuliwa baada ya Rais Samia kutoa skana moja kwa ajili ya upande wa Zambia.

Pia, Waziri Jafo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo kwa kutenga zaidi ya ekari 1,500 ambapo ekari 1000 ni kwa ajili ya bandari kavu na ekari 500 kwaajili ya ujenzi wa viwanda.

“Mkuu wa Mkoa (wa Songwe) nikuhakikishie tutafanya kila njia viwanda hivyo vitajengwa. Mheshimiwa Rais nikuhakikishie sisi Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na TRA pamoja na Forodha tutahakikisha vikwazo vyote visivyokuwa vya kikodi tuweze kuviondoa kwa lengo la kuhakikisha Tanzania hii inanufaika kwa suala la biashara” Amesema Dkt. Jafo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo wakati wakisubiri kumpokea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Tunduma Mkoani Songwe Julai 18, 2024.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe Farida Mgomi pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi Happiness Seneda wakati wakisubiri kumpokea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Tunduma Mkoani Songwe Julai 18, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtambulisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo kwa wananchi wa Tunduma Mkoani Songwe wakati wa Ziara yake Mkoani humo Julai 18, 2024.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mawaziri wenzake wakati
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliposimama na kusalimiana na Wananchi wa Tunduma Mkoani Songwe Julai 18, 2024 alipomaloza ziara yake ya kikazi Mkoani Rukwa.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizungumza Leo Julai 18, 2024 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliposimama kuwasalimia wananchi wa mji wa Tunduma Mkoani Songwe alipopita akitoka katika ziara yake Mkoa wa Rukwa

Related Posts