JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUZINI NA BINTI YAKE – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mfugaji na mkazi wa Kipata Kiromo Bagamoyo Yusuph Ngula Kitala (60), amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuzini na binti yake wa miaka 16.

Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Kibaha imemtia hatiani mtu huyo kwa kutenda kosa Hilo kinyume na Sheria na maadili ya kitanzania kwa binti mwenye umri wa miaka 16

Tukio Hilo lilitokea Kati ya mwezi Mei na Disemba 2023 huko Kipata wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ambapo mshitakiwa alidiriki kufanya mapenzi na binti wa miaka 16 ambaye ni mtoto wake mwenyewe.

Baada ya ushahidi kukamilika mtuhumiwa alitiwa hatiani kwa kosa hilo na kuadhibiwa kifungo Cha miaka 30 jela na Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Samera Suleiman Julai 17, 2024 katika Mahakama ya wilaya ya Bagamoyo.

#KonceptTvUpdates

Related Posts