Kongamano la Wanaume DSM, Mwenyekiti asema chakula bure “Mtakunywa supu, usafiri upo”

Katika hali ambayo haijazoeleka Mwenyekiti wa Wanaume Kanisa la CLGN lenye Makao Makuu yake Kinyerezi Dar es Salaam, Obadia Mushi amesema watatoa chakula bure katika kongamano litakalowahusu wanaume tu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kugawa vipeperushi, Mushi amesema ;

“Tukio litafanyika 20/7/2024 siku ya Jumamosi tutakuwa na kongamano la Wanaume litakalofayika Mbezi Beach Goigi, mnakaribishwa wote wanaume tujumuike kwa pamoja katika eneo la kukombolewa fikra, kushamiri kiroho na kimwili na kupata neno la Mungu,”

“Chakula ikiwemo supu kuanzia asubuhi na kuendelea ni msile nyumbani kwenu mje kula kanisani kwetu siku ya Jumamosi na usafiri upo,”.

Related Posts