Moshi. Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa amefikishwa mahakamani mkoani Kilimanjaro leo Alhamisi Julai 18, 2024 akisubiri kusomewa mashtaka mbalimbali likiwemo la uchochezi.
Tayari mawakili wake, Hekima Mwasipu na Dickson Matata wamefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.
Wengine waliopo katika viunga vya mahakama hiyo ni wafanyakazi wa taasisi yake, akiwemo James Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Kilawila pamoja na marafiki zake wa karibu.
Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusafirishwa hadi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na tuhuma tatu.
Malisa anakabiliwa na tuhuma tatu ikiwemo kuchapisha taarifa za uchochezi kuhusu mauaji ya Beatrice Minja, mkazi wa Rombo anayedaiwa kuuliwa na mtu aliyekujulikana kwa jina la Paul Tarimo na tukio la mwanafunzi anayedaiwa kuawa kwa kupigwa Moshi.
Tuhuma nyingine ni kutoa taarifa bila kibali kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu walimu waliokuwa wakisahihisha mitihani ya kidato cha nne Januari, mwaka huu na kutolipwa posho zao.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi