Manchester City imethibitisha kumsajili winga wa Kibrazil, Savinho kwa ada ya pauni milioni 21 itakayofikia milioni 33.6 pamoja na nyongeza akitokea Troyes ya Ufaransa.
Savinho (20) ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Girona ya Uhispania amesaini mkataba wa miaka mitano mpaka Juni 2029 na anakuwa usajili wa kwanza wa Man City majira haya ya kiangazi.
Msimu uliopita aliifungia Girona magoli 11 na kusaidia (assist) mengine 10 akiiongoza Girona kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya ilimaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Uhispania nyuma ya Real Madrid na Barcelona.
Savinho atavaa jezi namba 26 iliyokuwa ikivaliwa na Riyard Mahrez ambaye pia alikuwa akicheza kama winga wa kulia hivyo Mbrazil huyo anarithi jezi na nafasi ya Mahrez.