SIMBA NA YANGA KUCHUANA NGAO YA JAMII AGOSTI 8 – MWANAHARAKATI MZALENDO

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa Simba itacheza dhidi ya watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 8 saa moja usiku.

Mfumo huu wa kucheza Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii ni mara ya pili kutumika ambapo ulianza mwaka jana ambapo Simba waliibuka Mabingwa kwa kuifunga Yanga katika mechi ya Fainali.

Mshindi wa mechi yao atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union.

Kikosi cha Simba bado kinaendelea kupiga kambi nchini Misri kujiandaa na msimu mpya wa mashindano na kitarejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.

#KonceptTvUpdates

Related Posts