Ursula von der Leyen achaguliwa tena – DW – 18.07.2024

Ameahidi pia kuendelea na mpango wa Ulaya juu utunzaji mazingira pamoja na kupunguza mzigo wake kwa viwanda.  

Wabunge wa Bunge la Ulaya waliunga mkono hoja ya von der Leyen kugombea muhula mwingine wa miaka mitano katika usukani wa Ulaya, Baraza kuu la utendaji la Muungano kwa kura 401 zilizomuunga mkono na 284 kupmpiga katika kura ya siri iliyojumuisha wanachama 720.

Akitangaza matokeo hayo spika wa bunge la Ulaya RobertaMetsola amesema:

Kura za kupinga 284, ambao hawakupiga kura ni15, Kura 7 ziliharibika, Kwa mujibu wa matokeo haya, mgombea wa urais wa Halmashauri ya Ulaya, aliyependekezwa na Baraza la Ulaya amechaguliwa. Ningependa kumpongeza Ursula von der Leyen juu ya kuchaguliwa kwake tena, na ninamtakia kila la kheri kwa utekelezaji wa majukumu yake.”

Katika hotuba yake ndani ya Bunge la Ulaya mjini Strasbourg von der Leyen aliweka wazi mpango uliolenga ustawi na usalama, unaochangiwa na changamoto za vita vya Urusi nchini Ukraine, ushindani wa kiuchumi duniani na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ulinzi thabiti Ulaya

Umoja Ulaya- Ursula von der Leyen
Picha: Jean-Francois Badias/AP/picture alliance

Von der Leyen, waziri wa ulinzi wa zamani wa Ujerumani aliahidi kuunda “Umoja wa kweli wa Ulinzi wa Ulaya”, kwa kuanzia na miradi mikuu ya mtandao wa ulinzi wa anga. Mpango huo ulizua ukosoaji kutoka kwa Kremlin, ambayo ilisema  unaonyesha mtazamo wa kile ilichokitaka kama “matumizi ya jeshi na makabiliano”.

Aidh Von der Leyen alimkashifu Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban kwa ziara ya hivi majuzi  kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow kauli ambayo iliibua shangwe na  makofi kutoka kwa wabunge wa bunge la Ulaya.

Viongozi mbali mbali wamempongeza Ursula von der Leyen kwa kushinda muhula mwingine wa miaka mitano kama rais wa Tume ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk.

Kura za kupinga

Miongoni mwa waliopinga muhula wa pili kwa von der Leyen, ni chama cha Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni cha Meloni Brothers. Nicola Procaccini, mwenyekiti mwenza wa kundi la Wahafidhina wa Ulaya na Wanamageuzi (ECR) alisema Kupiga kura von der Leyen kungemaanisha kwenda kinyume na baadhi ya kanuni zao. 

 Straßburg 2024 |Bunge la Ulaya
Wabunge katika bunge la Ulaya wakipiga kura kumchagua rais wa Halmashauri kuu wa umoja huo.Picha: Johannes Simon/Getty Images

Hata hivyo kuchaguliwa tena kwake kunatoa mwendelezo katika Taasisi muhimu ya Umoja wa Ulaya wakati ikipambana na changamoto za nje na ndani – ikiwa ni pamoja na kuongeza msaada kwa upande wa kulia

na vyama vya siasa vinavyotumia sarafu ya Euro katika umoja huo wa mataifa 27.

Katika wiki zijazo, anatarajiwa kupendekeza makamishna wake, ambao watakabiliwa na vikao vya kibinafsi kutoka kwa wabunge kabla ya kura ya mwisho kwa Tume nzima baadaye mwakani.

 

 

Related Posts