WAHITIMU nchini wameshauriwa kujenga tabia kujiajiri pindi wanavyomaliza vyuo mbalimbali ili kusaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.
Rai hiyo imetolewa mapema leo jijini Dar es Salaam na na Mwenyeki wa Kamati ya Ufuatiliaji na ujifunzaji wanafunzi kutoka Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT), Dkt . Ambele Mtafya,wakati wa kuchukua maoni kutoka kwa wahitimu wa Chuo hicho juu hali ya soko la ajira lilivyo.
“Tunatamani wanafunzi wetu wajijengee utamaduni wa kujiajiri ili wanapojiajiri waweze kuwaajiri wenzao”amesema Dkt. Mtafya.
Aidha Dkt Mtafya amesema tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia sabini ya wahitimu wa chuo cha DIT wameajiriwa au kujiajiri huku asilimia 30 wakiwa bado hawajaajiri au kujiajiri.
“Ndio maana tumewaita wadau tuweze kujadili, kwanini asilimia 30 hizi wamekosa ajira, tujue tatizo ni mitahala au nini tubadilishe”amesema Dkt Mtafya.
Dkt. Mtafya ,amesema Chuo Cha DIT kimeweka utaratibu wa kuwafuatilia wahitimu wake kujua kama wameajiriwa na chuo hicho kinakwenda kwa waajiri kupata maoni yao kuhusu wahitimu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugezi wa Taaluma kutoka Chuo cha (DIT),Dkt Petro Tesha,amesema lengo la mkutano huo ni kupata maoni juu ya watahiniwa waliokuwa chuo hicho ili kuboresha mafunzo yao wanayotoa.
Dkt Tesha amesema baada kupata maoni hayo watarudi kuangalia mitaala yao je inaendana soko la ajira kwenye maeneo ya viwanda,teknolojia.