Dkt. Tulia Ackson,awasili Delhi-India kwa ziara ya kikazi

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 19 Julai, 2024 amewasili Jijini Delhi Nchini India kwa ziara ya kikazi.

Dkt. Tulia amepokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Bunge la India, Balozi Anjani Kumar pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini India, Mhe. Anisa Mbega ambapo anatarajia kutembelea Bunge la Nchi hiyo na kutoa Mhadhara kuhusu Demokrasia na Diplomasia ya Kibunge mapema wiki ijayo.

Related Posts