Israel yaendelea kuvurumisha mashambulizi ya ardhini Gaza – DW – 19.07.2024

Katika vita hivyo vilivyodumu kwa takriban miezi kumi sasa kuanzia juma lililopita Israel imeongeza mashambulizi ya anga na ardhini na kuuwa watu kadhaa.

Wakaazi katika eneo hilo ambao wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi wamesema kwamba jeshi la Israel wameyalipua makaazi kadhaa katika muda wa siku tatu zilizopita.

Maafisa wa afya wa Palestina walisema watu wanane waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya anga ya Israel kwenye nyumba mbili mapema leo huko Nuseirat.

Nako katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza Rafah, Israel imesema inalenga kusambaratisha kituo cha mwisho cha kijeshi cha Hamas. Wahudumu wa afya wanasema watu watano waliuwawa na miili yao ilihamishiwa katika hospitali karibu na mji wa Khan Younis.

Soma pia:Israel yashambulia eneo la katikati mwa Gaza wakati likiendelea kuingia Rafah

Eneo la Mawasi ambalo lilitangazwa na israel kama eneo salama na kuwataka Wapalestina kuelekea huko kwa ajili ya kujihifadhi na mapigano yanayoendelea, wakaazi wanasema si salama tena kutokana na mkururo wa mashambulizi ya Israel inayosema yanawalenga wapiganaji wa Hamas.

shambulio la Tel Aviv ni awamu mpya ya operesheni za Wahouth?

Katika hatua nyingine Waasi wa Kihuthi ambao wamedai kuhusika na shambulio la hatari la droni mapema leo mjini Tel Aviv wameunda ndege zisizo na rubani zenye uwezo mkubwa wa kushambulia.

Israel, Tel Aviv | watu wakishuhudia shambulio la alfajir
Baadhi ya watu wakiangalia namna ambavyo jengo lilivyoharibiwa baadha ya shambulio linalodaiwa kufanywa na WahouthPicha: Ricardo Moraes/REUTERS

Tangu Israel ianzishe mashambulizi ya kulipa kisasi dhidi ya Hamas baada ya shambulio la Oktoba 007, waasi Wakihuthi wanaoungwa mkono na Iran wamefanya mashambulizi kadhaa ya droni na makombora dhidi ya meli katika Bahari shamu na Ghuba ya Aden, katika kile wanachosema ni kuonesha  mshikamano kwa Wapalestina.

shambulio la leo alfajir linatjwa kuashiria “awamu mpya” ya operesheni za Wathuthi  dhidi ya Israeli, ambao wamekuwa wakiendeleza uwezo wao wa ndege zisizo na rubani tangu 2014 walipouteka mji mkuu wa Yemen Sanaa.

Soma pia:Shambulio la droni laua mtu mmoja Tela Aviv

Msemaji wa Jeshi la Israel Danie Hagari amesema wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu shambulio hilo na kuangalia ni majibu ya aina gani yanahitajika ili kulinda usalama na maslahi ya Israel.

“Tuko kwenye vita vya pande nyingi. Tunafanya kazi kwa pande zote na kutetea nchi kila siku. Baadhi ya pande hizi ziko karibu na zingine ziko mbali. Tunafanya kazi dhidi ya vitisho vyote.” Alisema Hagari baada ya shambulio la alfajir.

Aliongeza kwamba “tunafanya uchunguzi kujua ni wapi hasa kitisho kimetokea na majibu gani yanahitajika na dhidi ya nani anaetishia taifa la Israel.”

Wahouthi walidai ndege zao mpya zisizo na rubani zinaweza kupita mifumo ya ulinzi ya anga ya Israeli, walakini, jeshi la Israel limesema kwamba droni hiyo iliyokuwa na vilipuzi iligunduliwa siku ya Alhamisi na kuhusisha shambulio hilo na “makosa ya kibinadamu.”

ICJ: Israel inakalia maeneo ya Wapalestina kinyume na sheria

Kando na mashambulizi hayo ya kulipa kisasi ya kila upande nako kwenye uwanja wa sheria na haki, Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa ICJ imetoa ushauri wake wa kisheria ikisema, ukaliaji wa Israel katika maeneo ya Wapalestina ni kinyume na sheria na inapaswa kukomeshwa haraka iwezekanavyo.

Israel epusheni mauaji ya halaiki Gaza

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Maoni hayo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, ingawa hayana nguvu kisheria, yataongeza shinikizo la kisiasa la kimataifa kwa Israel. Israel iliondoka Gaza mwaka 2005 lakini inaendelea kudhibiti mipaka ya ardhi na bahari ya eneo hilo la pwani, pamoja na anga yake.

Idadi ya walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ambao uko kati ya kitovu cha Israel na Jordan, wakati huo huo imeongezeka hadi karibu nusu milioni. Ikiwa ni pamoja na Jerusalemu ya Mashariki,

 

Related Posts