Simba Queens yajichimbia Bunju | Mwanaspoti

MABINGWA wa Ligi ya wanawake (WPL), Simba Queens imeanza kambi ya kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikijichimbia Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju, jijini Dar es Salaam.

Msimu wa 2022, Simba ilichukua ubingwa huo wa Cecafa kwa kuifunga She Corporate FC ya Uganda kwa bao 1-0 na kukata ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika iliyoshika nafasi ya nne baada ya kuwa kati ya timu nne zilizotinga nusu fainali, japo ilipoteza 1-0 na Bayelsa Queens ya Nigeria katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa kikosi hicho, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema wameingia mapema kambini ili kujiweka fioti kabla ya kuanza vita ya Cecafa kupata uwakilishi wa michuano ya CAF ambayo hesabu zao ni kufanya vizuri zaidi na ilivyokuwa mwaka wao wa kwanza kule Morocco.

Mgosi alisema wameingia kambini wakiwa na baadhi ya wachezaji huku wengine wawili, Aisha Mnunka na Violeth Nickolaus watajiunga na timu baada ya kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa ‘Twiga Stars’.

“Aisha na Violeth watajumuika na wenzao baada ya kutoka Tunisia kwenye majukumu ya timu ya taifa tumeingia kambini mapema kutokana na ushindani wa mashindano hayo,” alisema Mgosi, nahodha wa zamani wa timu ya wanaume ya Simba aliyewahui pia kuwika na JKT Tanzania, Mtibwa Sugar, DC Motema Pembe ya DR Congo na Taifa Stars.

Msimu uliopita kwa michuano ya Cecafa, JKT Queens ndio iliyobeba ubingwa kwa penalti 5-4 dhidi ya CBE ya Ethiopita na kuikata tiketi ya CAF ikiwa timu ya tatu kwa ukanda huo baada ya Vihiga Queens ya Kenya na Simba, lakini iliishia makundi, huku taji likienda kwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoinyoosha Raja Casabalanca kwa mabao 3-0.

Related Posts