Ikiwa ni mwendekezo wa Kampeni ya Kitaifa Kuhamasisha Uwekezaji wa Ndani imeendesha semina juu ya masuala ya mbalimbali ya Uwekezaji leo 19 Julai, 2024 katika Ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amepongeza jitihada zilizofanywa na Mkoa wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda katika uwekezaji na kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa Mkoa namba mbili nchini kwa uwekezaji.
Amesema hayo alipozungunza na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa mwanza alioshiriki semina
Kampeni maalum kuhamasisha uwekezaji wa ndani inaratibiwa na TIC mikoa yote Tanzania ambapo leo wako Jijini Mwanza