WALIOFOJI SAHIHI SAKATA LA YANGA WAKIBAINIKA KIFUNGO CHA MAISHA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Kufuatia sakata la Viongozi wa Yanga kutakiwa kuachia madaraka baada ya baadhi ya Wazee wa Club hiyo kushinda kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wakili wa Mahakama kuu Dedan Kapongo ametolea ufafanuzi wa kisheria kuhusu tuhuma zilizosemwa na Mkurugenzi wa sheria wa Yanga kwamba Wazee hao waligushi sahihi za baadhi ya Viongozi wa Yanga ili iwe rahisi kwao kushinda kesi hiyo.

 

 

 

Wakili Kapongo amesema Mtu anayegushi nyaraka na kuidanganya Mahakama au Taasisi huenda akapata adhabu ya miaka saba “kufoji ni kosa la jinai na sio kosa la madai, zaidizaidi ni kosa la jinai ambalo litaanzia Polisi ambao watafanya uchunguzi, kuna aina nyingi za kufoji ambapo kufoji nyaraka yoyote ambayo ni rekodi ya Mahakama utafaungwa kifungo cha maisha”

 

 

 

“Ile kitu ambayo alikua anaongea Mwanasheria wa Yanga nimeona anaonesha document ambayo ilipelekwa Mahakamani ikionesha kwamba ni utetezi wa upande wa Yanga na akionesha kwamba zile sahihi zilikua zimefojiwa, ile tunaiweka upande wa rekodi ya Mahakama kama umefoji document yoyote ya rekodi ya Mahakama maana yake wewe unafungwa kifungo cha maisha”

 

 

Chanzo : Millard Ayo

 

Related Posts