Wananchi mkoani Mtwara watakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika visiwa vya Comoro

Wananchi mkoani Mtwara wametakiwa kuchangamkia fursa ya biashara ya bidhaaa mbalimbali katika visiwa vya Comoro kwa kulima bidhaa za mbogamboga na mikunde kwa kuwa uhitaji ni mkubwa katika taifa hilo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenan Sawala wakati anazindua mradi wa kuongeza mrejesho jumuishi na kujenga ustahimivu kwa jamii zilizoathiriwa na mafuriko na kilimo cha bustani mkoani Mtwara.

Amesema wananchi wazalishe mazao mbalimbali yatokanayo na bustanu ikiwemo ya muda mfupi ili wajipatie fedha kwa haraka kupitia soko la ndani au nje ya nchi.

Ameeleza kukosekana kwa bidhaa za uhakika ambazo zinaweza kusafirishwa nchi ya Comoro kumepelekea kuwepo kwa utaratibu wa muda mfupi wa upatikanaji wa meli inayosafirisha bidhaa visiwa vya Comoro, wastani usipungua mara mbili kwa mwezi.

“Mheshimiwa Rais ameingua Mtwara, sasa sisi tufungue macho kuona fursa zilizopo ili tujiletee maendeleo, ametuletea miradi ya kimkakati kwa mfano upanuzi wa bandari ya Mtwara, tuitumie katika kujinufaisha” amesema Kanali Sawala

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi wa Shirika la Sugec ambalo linatekeleza mradi huo chini ya Usimamizi shirika la Kimataifa la Maendeleo la UNDP kwa ufadhili wa serikali ya Japan, Revocatus Kimario amesema mkoa wa Mtwara umekuwa ukiagiza bidhaa mbalimbali kutoka katika mikoa mengine na wastani wa kiasi cha shilingi milioni 400 kinatumika kwa wiki kuagiza bidhaa.

Amesema iwapo jamii watachangamkia fursa za utekelezaji wa mradi huo utachangia kuongeza uzalishaji wa bidhaa kama choroko, nyanya, hoho, vitunguu na bamia.

Related Posts