CHAGUENI VIONGOZI WA MAENDELEO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA – DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuchagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwenye uchaguzi mwaka huu ambao watakuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo na kutatua changamoto zao kwa haraka.

Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara kijiji cha Lyambamgongo wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

“Muda utakapofika tuwe tayari kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili tuweze kuchagua viongozi wazuri wenye sifa za kuchaguliwa ambao watasaidia kuleta maendeleo, tunataka jimbo la Bukombe libadilike kwa kuwa na watu wenye maono au mawazo mazuri yatakayosaidia utatuzi wa changamoto zinazotukabili”, amefafanua na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Related Posts