JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MITANO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani, Haji Mustapha (20) mkazi wa mtaa wa FFU Bar Mpya, kata ya Muriet Jijini Arusha baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano (05).

Akisoma hukumu hiyo kesi namba 138 ya mwaka 2023 Julai 22, 2024 Hakimu wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Marando alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Septemba 20, 2023 muda wa usiku huko katika mtaa wa FFU Bar Mpya, Kata ya Muriet Jijini Arusha kabla ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia.

 

Related Posts