Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:-
-
B.i Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
-
Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Bw. Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.
-
Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Bi. Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).
Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu