RAIS SAMIA ATENGUA TENA VIGOGO HAWA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Viongozi mbalimbali akiwemo Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Rais amemtengua pia Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.

Wengine waliotenguliwa ni Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USAF) na Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

 

Related Posts