RODRI ASHITAKIWA NA UEFA KISA HIKI HAPA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Nyota wa Manchester City na Uhispania Rodri, ameshtakiwa na UEFA baada ya kutoa kauli ya kuudhi kuhusu Gibraltar wakati wa kusheherekea ushindi wa EURO 2024.

Kiungo huyo alisikika akiimba ”Gibraltar ni ya Uhispania” kupitia kwenye kipaza sauti mbele ya maelfu ya Mashabiki katika shughuli moja iliyofanyika huko Madrid Julai 15.

Mwingine aliyeshtakiwa ni nahodha wa Uhispania Alvaro Morata. Matendo ya wawili hao yalisababisha malalamiko rasmi kutoka Shirikisho la soka la Gibraltar (GFA) ambayo yalikiitaja kitendo hiko kuwa ni cha kuudhi sana.

Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji hao wamevunja sheria za heshima za UEFA kwa kutumia shughuli ya michezo kutoa dhihirisho lisilohusiana na michezo, na kuuletea mchezo sifa mbaya.

Gibraltar ni eneo la ng’ambo la Uingereza ambalo Uhispania inadai umiliki wake. Hatima ya eneo hilo ni suala nyeti la kidiplomasia.

Related Posts