SIMBA KUZINDUA JEZI KESHO MOROGORO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Klabu ya Simba SC imepanga kuzindua jezi zake za msimu wa 2024/2025 ndani ya Hifadhi ya Mikumi, Mkoani Morogoro kesho.

 

 

Simba SC watazindua jezi hizo walizoziita jina na Ubaya Ubwela ndani ya hifadhi hiyo na maandalizi yote kwa ajili ya shughuli hiyo yamekamilika.

 

 

Msimu uliopita Simba SC ilizindua jezi zake katika Mlima wa Kilimanjaro, Jijini Arusha. Licha ya Simba SC kwenda kuzindua jezi ndani ya hifadhi hiyo, lakini pia watatumia mbuga hiyo kuzindua rasmi hamasa za kuelekea katika kilele cha Simba Day, Agosti 3.

 

Related Posts