Simba yatoa msimamo ishu ya Kibu Denis

Uongozi wa Simba umepanga kumchukulia hatua za kinidhamu kiungo wake mshambuliaji, Kibu Denis kutokana na kushindwa kuwasili kwenye kambi ya timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine itakayoshiriki msimu ujao na badala yake amekuwa akitoa sababu tofauti kila siku.

Simba kwa sasa iko jijini Ismailia, Misri ilikoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, huku mchezaji huyo hadi sasa bado hajaripoti.

Taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo leo Julai 23 , imeeleza sababu za mchezaji huyo kitojiunga na kambi ya timu hiyo hadi sasa.

“Klabu ya Simba inautaarifu umma, mchezaji wake Kibu Denis Prosper hajaripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024-2025.”

“Tunapenda kuutarifu umma, Simba tulimwongezea mkataba Kibu wa miaka miwili zaidi uta-kaoisha Juni 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimkataba,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza;

“Hata hivyo mchezaji huyu amekuwa akitoa sababu kadha wa kadha zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini na kutokana na utovu huu wa nidhamu, klabu itamchukulia hatua stahiki za ki-nidhamu na umma utapewa taarifa,” mwisho wa kunukuu taarifa hiyo.

Related Posts