Bodi ya TASAC yabaini Changamoto Katika Bandari ya Bagamoyo

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) Nahodha Mussa Mandia akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kupunguza kodi katika bidhaa za Kutengenezea Boti ambayo iko nyuma yake wakati Bodi ilipofanya ziara katika Bandari ya Bagamoyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Mohamed Salum akionesha Vyombo Vidogo vya Majini katika Bandari ya Mbegani wakati Bodi ya TASAC ilipotembelea Bandari hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli  Tanzania (TASAC) Mohamed Salum akizungumza Bodi ya TASAC wakati Bodi hiyo  ilipotembelea Bandari Mbegani wilayani Bagamoyo.

Afisa Bandari wa Bandari ya Bagamoyo  David Kasembe akitoa  maelezo Kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia wakati Bodi hiyo ilipotembelea Bandari ya Bagamoyo.

Afisa Forodha Clara Melekzedeck akitoa maelezo kwa Bodi ya TASAC ilipotembelea Bandari ya Bagamoyo.

*Yaweka mikakati ya kukutana na TPA na TRA katika uboreshaji wa Bandari hiyo.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

BODI ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema Kupwa na kujaa kwa maji katika Bandari ya Bagamoyo imetajwa kuwa changamoto inayokwamisha ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Bandari hiyo.

Hayo yamebanishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC Nahodha Mussa Mandia wakati wa ziara ya Bodi ya TASAC kukagua ufanisi wa Bandari Bagamoyo,mkoani Pwani.

Amesema Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana katika usafirishaji bidhaa mbalimbali kwenda Zanzibar hivyo lazima iangaliwe katika miundombinu ya kufanya kazi kwa ufanisi kuliko ilivyosasa maji ya kikupwa hakuna shughuli zinazofanyika.

Amesema kuwa Bodi itakutana na TPA juu ya kuishauri kuchimba kwa ajili vyombo vidodgo viweze kuendelea kufanya kazi hata kama maji ya bahari yakiwa yamekupwa.

“Ipo haja ya miundombinu ya Bandari hiyo kufanyiwa maboresho makubwa ili kuruhusu Vyombo kufanya kazi muda wote na kuruhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali”amesema Nahodha Mandia.

Amesema Bodi katika ziara ya Bod kutoa ushauri katika kuhakikisha Bandari zote zinafanya kazi kwa tija na kusaidia Serikali kuongez mapato yanayokwenda kutoa huduma kwa wananchi.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa Bandari ya Mbegani ikikamilika vyombo vidogo vya usafirishaji majini vitaongezeka.

Bandari ya Bagamoyo ufanisi mdogo kutoka na changamoto mbalimbali zinazohitaji kupatiwa muarobaini baada ya na TPA kuwekea mkakati wa changamoto hizo.

Mbali na changamoto ya kujaa na kupwa kwa maji kwenye bandari hiyo baadhi ya wavuvi wanaiangukia Serikali kuhusu kodi ya malighafi ya kukarabati boti.

Hata hivyo bodi ya TASAC imeweka wazi mpango wa kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ili kupata Suluhu ya namna ya kupunguza gharama hizo ili kufanya kuwepo kwa boti nyingi zitazochangia mapato kuliko kutegemea kodi ya uingizaji bidhaa hizo.

Nahodha Mandia amesema kuwa changamoto nyingine ni bandari kukosa uzio na kufanya kuwepo na mwingiliano usio na tija pamoja na Bandari kukosa Taa.

Related Posts