● Bolt imeongeza ufanisi wa programu ya dereva ili kutambua utendaji kazi na kuwapa madereva zawadi.
Dar es Salaam, 23rd Julai 2024 – Bolt, kampuni inayoongoza kwenye huduma ya taxi mtandao Africa, imezindua Tuzo za Bolt, Dhumuni la tuzo hizi ni kutambua huduma bora inayotolewa na madereva kwenye huduma ya taxi mtandao.Tuzo hizi zitatolewa kwa mfumo wa madaraja mbali mbali na pia punguzo za kwenye programu ya madereva. Bolt inatumia Tuzo hizi kuwashukuru madereva wake na kuwapa motisha.
Madereva wataunganishwa moja kwa moja katika tuzo za Bolt na watajipatia pointi kulingana na idadi ya abiria waliowasafirisha katika kipindi cha mwezi mmoja. Kuna viwango vinne vya zawadi kulingana na alama zilizokusanywa ikiwa ni pamoja na Bronze, Silver, Gold na Platinum. Tuzo za Bolt zitasaidia kuwatambua na kuwatuza madereva washirika, kwa motisha na mapunguzo ambayo huwasaidia madereva kudhibiti gharama zao za uendeshaji na kurekebisha gharama zisizotarajiwa.
Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu, Bolt Tanzania alisema: “Kama Bolt, tunatambua kuwa dereva akiridhika atamsafirisha na kumfikisha abiria aliyeridhishwa. Tukiwa na Tuzo za Bolt, tunalenga kutambua na kuwatia moyo madereva kwenye mifumo yetu ambao wanafanya safari mara kwa mara. Mpango huu unaangazia dhamira yetu ya kuboresha ufanisi wa programu ya dereva na kuthamini jumuiya ya madereva wa taxi mtandao.”
Tuzo za Bolt inaungana na msururu wa uboreshaji wa hivi karibuni wa programu za Bolt kwa madereva ikiwa na lengo la kusaidia madereva kutoa huduma ya hali ya juu kwa abiria. Kipengele kipya cha tuzo za Dereva huwapa madereva utambuzi wa huduma ya kipekee na motisha kupitia pongezi na maoni chanya za ukadiriaji wa baada ya safari. Bolt inaendelea kutoa fursa rahisi zaidi za mapato kwa madereva, na kuhakikisha abiria wanaweza kupata huduma zetu popote walipo.