DKT. TAX AKUTANA NA KAIMU NAIBU WAZIRI WA MAREKANI

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), akisalimiana na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipokutana naye kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Batle alipomsindikiza Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaamm, kulia ni Katibu Mkuu Balozi Shelukindo akisalimiana na Balozi wa Marekani Mhe. Michael Batle

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), akizungumza na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) akiwa na watumishi wa wizara katika kikao kati ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Batle (kulia) akiwa na ujumbe wake katika kikao kati ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiwa na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akiwa na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass pamoja na Katibu Mkuu Balozi Samwel Shelukindo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Batle (kulia) alipofika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika picha ya pmoja baada ya kumaliza mazungumzo yao katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb), amekutana kwa mazungumzo na Kaimu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Siasa wa Marekani Mhe. John Bass katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Dkt. Tax amemuhakikishia Mhe. Bass kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Marekani katika masuala yenye manufaa kwa nchi hizi mbili na wananchi wake.

Amesema ziara ya Mhe. Bass nchini ni ushahidi wa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili huku ikonesha umuhimu mkubwa katika kuendelea kudumisha na kuimarisha maelewano, ushirikiano na urafiki kati ya Tanzania na Marekani na kuongeza kuwa kwa miaka mingi kumekuwa na majadiliano ya wazi kwa ajili ya kujenga na kuweka misingi ya ushirikiano madhubuti kati ya Tanzania na Marekani.

“Nina Imani kuwa kupitia ushirikiano na uhusiano wetu sio kwamba tutakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja bali pia tutanufaika na fursa zilizopo mbele yetu ili kuchochea ukuaji na ustawi wa pamoja, alisema Dkt. Tax.

Naye Mhe. Bass akizungumza katika kikao hicho amesema ziara yake nchini ina lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Tanzania na kuahidi kuwa Marekani inaiona Tanzania kama mdau wa kimkakati katika ushirikiano wa maendeleo.

Ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya Marekani na kuongeza kuwa ni matarajio yake kuwa kupitia majadiliano mbalimbali ambayo yemekuwa yakifanyika yatasaidia nchi yake kuibua kwa undani maeneo muhimu ambayo Serikali ya Tanzania inahitaji kuendelea ushirikiana na Marekani.

Tanzania na Marekani zimekuwa zikishirikina katika nyanja za afya kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la USAID, elimu, kilimo, biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama.

Related Posts