JUMLA YA TSHS 4, 780,000/= KUCHANGIA MAENDELEO VIJIJI VYA KIFANYA, LWANGU NA UTENGULE

JULAI 18, 2024, Mhe. Deo Mwanyika (MB) akiwa katika ziara kata ya Kifanya amewapongeza wananchi wa vijiji vya Kifanya, Utengule na Lwangu kwa kuchangia na kuendeleza shughuli mbalimbali za ujenzi katika vijiji vyao kama ujenzi wa shule shikizi kitongoji cha ITENGULE – KIFANYA, shule shikizi MZALENDO – LWANGU na ujenzi wa nyumba ya Mtendaji kijiji cha UTENGULE.

Mhe. Deo Mwanyika amewa changia Tripu 10 za mawe ujenzi wa shule shikizi ITENGULE zenye thamani ya Tshs 1,300,000, saruji mifuko 30 (Tshs 555,000) ujenzi wa nyumba ya Mtendaji kijiji cha Utengule, saruji mifuko 20 (Tshs 370,000/=) ujenzi wa shule shikizi Mzalendo – Lwangu.  Chanzo cha fedha:- Fedha binafsi.

Pia Tenki  la maji shule ya Msingi Msindu lenye thamani  ya Tshs 2,000,000/  na saruji mifuko 30 (Tshs 555,000/=) shule shikizi Mzalendo – Lwangu zitatolewa kupitia Mfuko wa jimbo.

Mwisho, Mhe. Mbunge amewaasa wananchi kuendelea na moyo ya kuchangia  shughuli mbalimbali za maendeleo na serikali itaendelea kutoa fedha  katika ujenzi huo. Serikali imeendelea kuunga mkono juhudi za wananchi kwa kutoa fedha katika Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Maji, Barabara na Umeme ikiwa lengo kuu ni kumsogezea huduma bora mwananchi katika maeneo yao.


 

 

Related Posts