Kampuni ya Koncept Group yasheherekea Miaka 9 ya Ufanisi, yaahidi Makubwa kwa Wadau wake – MWANAHARAKATI MZALENDO

Kampuni ya Koncept Group chini ya Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Krantz Charles Mwantepele kwa kushirikiana na wadau wake imeandika historia ya kusherehekea miaka 9 ya mafanikio ya kiutendaji yenye ufanisi wa hali ya juu huku aikiahidi kuendelea kushirikiana na kutoa huduma bora kwa wadau wake.

Kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 2015 inajihusisha na Masuala ya Mawasiliano, Mahusiano ya Umma, Matangazo, Masoko ya Kidijitali, Uwakala wa Bima, Ulinzi na biashara ya ‘Real Estate’ kwa sasa imeandika historia kubwa ya Kimafanikio kupitia shughuli mbalimbali ambazo wanazifanya.

Koncept imefanikiwa kufanya kazi nzuri na makampuni mengi (wateja) hapa nchini tanzania kama vile NBC BANK, TIGO, SERENGETI BREWERIES, VODACOM, CRDB BANK, HISENSE, BETPAWA, DANUBE, KERRY, KOBE MOTORS, WORLD BANK, AKIBA COMMERCIAL BANK, TORANJ na pia kampuni baadhi kutoka nje (za kimataifa) kama vile THE BIG BAD WOLF (BBW).No alt text provided for this imageNo alt text provided for this image

Related Posts