Mecky ajipa matumini Dodoma Jiji

DODOMA Jiji FC inaendelea na kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, lakini kuna kitu amekisema kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Maxime.

Katika mazungumzo na Mwanaspoti, kocha huyo ameonyesha kufurahishwa na viwango vya nyota wake, huku akifurahishwa na siku chache ambazo wameweka kambi mkoani hapa.

Timu hiyo imeweka kambi jijini Arusha ikitazamiwa kuihamishia Morogoro, lengo ikiwa ni kuhakikisha wanajiweka fiti zaidi kabla ya kuanza kwa mashindano.

Maxime alisema kwa siku nane ambazo timu hiyo imeweka kambi Arusha kuna mabadiliko yameon-ekana ikiwemo miili ya wachezaji kuanza kuachia.

Alisema timu ni mpya kwa maana ya usajili wa wachezaji wapya wengi huku wale wa zamani wakibaki wachache, hivyo kazi ambayo anafanya ni kuhakikisha wanafanya mazoezi ya kujenga miili na timu ya ushindani.

“Maendeleo kwa sasa sio mabaya tunakwenda vizuri. Tayari kuna mwonekano mbele unakwenda vi-zuri,” alisema Maxime.

Akizungumzia ligi alisema anaamini itakuwa ngumu, lakini matarajio yake ni makubwa kufanya vizuri kutokana na wachezaji alionao na ikiwezakana kutwaa ubingwa ili kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kima-taifa.

Naye Francis Mkanula, kocha wa viungo wa timu hiyo alisema katika kuweka miili ya wachezaji sawa tayari wamefanya mazoezi ya gym ambayo ni muhimu katika kipindi hiki.

“Juzi tumecheza mechi ya kirafiki (dhidi ya Royal SC ya Daraja la tatu Mkoa wa Arusha) na kila mchezaji alipata dakika kadhaa za kucheza, tukaona ni vyema twende gym kwa ajili kurudisha sawa miili ya wachezaji,” alisema.

Related Posts