Moto wateketeza vibanda Stendi ya Msamvu

Moto umezuka usiku wa kuamkia leo na kuteketeza baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara wadogo pembezoni mwa Kituo Kikuu cha Mabasi, Msamvu mjini Morogoro.

Moto huo unaodaiwa kuanza saa 3:15 usiku kwa mujibu wa mashuhuda, umesababisha uharibifu kwenye vibanda takriban vinane.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro, Mrakibu Msaidizi Daniel Miala amesema chanzo cha moto huo ulioathiri vibanda kama vinane au tisa, hakijajulikana.

“Tulipokea taarifa ya uwepo wa moto katika eneo la stendi ya mabasi Msamvu. Tukafika hapa na magari mawili ya kuzima moto, tulikuta unaunguza vibanda kama nane au tisa, tukavizima ili visije kuharibu vingine.

“Mpaka sasa hatujajua chanzo cha moto huo, lakini tutaendelea kushirikiana na wadau wengine kufanya uchunguzi kubaini chanzo chake na tathmini ya uharibifu,” amesema Miala.

“Ukiangalia hapa kuna vibanda kama 60 na kama tusingeudhibiti moto mapema, vingeweza kuungua hata vibanda 50. Tunawashukuru wananchi kwa kutoa taarifa mapema.”

Mashuhuda wa tukio la moto huo wamelipongeza jeshi hilo kwa kufika mapema na kusaidia kuzima moto huo.
Wame huenda chanzo ni moto wa kupikia ambao haukuzimwa vizuri huku wengine wakidai ni hitilafu ya umeme.

Related Posts