Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua atembelea CATC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua ametembelea Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) na kukutana na menejimenti ya chuo hicho.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Julai 24,2024, Dkt. Mwinyimvua amepata fursa ya kutembelea na kujionea miundombinu ya chuo ya sasa ilivyo. Chuo cha CATC kinatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kisasa wenye gharama ya takriban shilingi bilioni 78 hadi kukamilika kwake ambapo Serikali inagharamia kwa asilimia mia moja mradi unaotegemewa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, Mkuu wa chuo cha CATC Aristid kanje aliishukuru serikali kwa kuubeba kwa uzito mradi wa uboreshwaji wa CATC kwa kutenga fedha ili kuhakikisha unatekelezwa kikamilifu. Na pia alitumia fursa hiyo kumueleza namna chuo cha CATC kilivyopata ithibati mbalimbali za ndani na nje ya nchi zinazokifanya chuo hicho kuwa cha Kimataifa.

Miongoni mwa ithibati za CATC ni pamoja na ISO 9001: 2015 Certified, ICAO TRAINAIR PLUS Full member Gold, Full Accredited by National Council for Technical and Vocational Education and Training (NACTVET), Approved Training Organization by Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), Council Member of African Aviation Training Organization (AATO), Corporate Member of Chartered Institute of Logistics and Transport (CILT) na Aviation Security Training Centre (ASTC-Dar es Salaam)

Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania ni moja kati ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua akizungumza na uongozi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) alipotembelea Chuo hicho ili kujionea miundombinu pamoja na kujitambulisha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua akipata maelezo kutoka Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje alipotembelea chuo hicho kilichopo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua akisaini kitabu cha wageni mara baada ya maelezo kutoka Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje alipotembelea chuo hicho kilichopo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua akitembelea maeneo mbalimbali ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje mara baada ya kutembelea chuo hicho kilichopo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Flora Alphonce akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje mara baada ya kutembelea chuo hicho kilichopo chini ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua (watano kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Flora Alphonce (wanne kushoto), Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje ( watano kulia) pamoja na watumishi wa CATC alipotembelea chuo hicho.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCAA Dkt. Hamis Mwinyimvua akiagana na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje mara baada ya kutembelea chuo hicho

Related Posts