Rais wa Kenya William Ruto amemteua gavana wa zamani wa kaunti ya Mombasa, Hassan Ali Joho kuwa waziri wa madini na masuala ya bahari, katika uteuzi wa majina mapya ya mawaziri alioutangaza hivi punde.
John Mbadi wa chama cha ODM ndiye atakayekuwa waziri mpya wa fedha.
Aliyekuwa waziri wa usafiri na miundombinu Kipchumba Murkommen, amehamishwa katika wizara inayoshughulikia masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo.
Joho na Mbadi ni miongoni mwa vigogo wanne wa upinzani waliojumuishwa katika baraza jipya la mawaziri huku Ruto akiahidi kuyataja majina mengine ya mawaziri muda mfupi ujao.