RC PWANI AKABIDHI MAGARI MAPYA KWA DC KISARAWE NA DC BAGAMOYO

NA VICTOR MASANGU,PWANI

Mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amekabidhi Magari mawili mapya kwa wakuu wa Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa kuwahudumia wananchi wao kwa urahisi zaidi.

Akikabidhi Magari hayo kwa wakuu hao wa Wilaya Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani amemshukuru kwa dhati Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Magari hayo yatakayokuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la usafiiri kwa wakuu hao wa Wilaya.

Kunenge alisema kupatikana kwa magari hayo mapya kutaweza ni juhudi kubwa ambazo amezifanya Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anaboresha mazingira ya kazi kwa wakuu wake wa Wilaya.

Alisema katika Mkoa wa Pwani kuna jumla ya Wilaya sana na kwamba Rais kwa awamu hii ameshatoa magari mapya matatu ambayo mawili yamekabidhiwa leo rasmi na mengine yatakabidhiwa katika awamu nyingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amempongeza kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia magari hayo ambayo yatakwenda kuwa msaada mkubwa.

Magoti alisema kwamba hapo awali alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kutumia gari nyingine lakini kwa sasa anashukuru kupata gari jipya ambalo litamuwezesha kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.

“Kwa kweli napenda kumshukuru kwa dhati Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais wangu Dkt.Samis Suluhu Hassan kwa kuweza kutupatia magari haya ambayo kwa kweli mm nilikuwa naenda vijijini kwa usafiri wa gari aina ya Pick up,:alisema Magoti.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash hakusita kumpongeza Mkuu wa Mkos wa Pwani kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na Rais Samia kuwapatia magari mapya kwa ajili ya kurahisisha usafiri na utekelezaji wa majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.





Related Posts