SAKATA LA KESI YA DITTO LAMECK DHIDI YA DSTV MAMBO YAKO HIVI – MWANAHARAKATI MZALENDO

#BURUDANI; Msanii Ditto alifungua kesi ya madai Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam mwaka 2020 akiomba Mahakama iamuru Multchoice Tanzania imlipe fidia ya shilingi bilioni 6 kwa kutumia wimbo wa “Nchi Yangu”

aliodai ni wake katika matangazo yao bila ridhaa yake.

Dstv walitumia wimbo huo katika kampeni za mataifa ya Afrika (Afcon) 2019 Ditto ameomba pia mahakama iamuru Dstv imlipe milioni 200 kutokana na Madhara ya jumla.

Pia ameomba Mahakama alipwe fidia ya asilimia 25% tangu siku alipofungua shauri hilo akidai kampuni hiyo imemnyima fursa ya kunufaika na kazi yake.

Katika kesi hiyo, Ditto alipeleka mashahidi watano na DStv ilikuwa na mashahidi wawili, Astrid Mapunda na Johnson Mshana wakiongozwa na mawakili, Simon Lyimo na Thomas Mathias.

Upande wa Ditto, baadhi ya mashahidi wake walikuwa ni mtayarishaji wa wimbo huo, Emmanuel Maungu (Emma the boy), meneja wake, Rodney Rugambo na Angela Karashani wakiongozwa na mawikili, Ally Hamza na Elizabeth Mlemeta.

Ditto Lameck hajafua Dafu kwenye hii kesi

Mahakama kuu imeshindwa kumtia hatiani Mdaiwa (Dstv) kwa Madai kuwa hawakutumia Original Version ya nyimbo ya Ditto bali alitumia second version ambayo ilitumika kwenye urithi Festival.

Wacha Tusubiri nakala ya Hukumu tuichambue.

Source; Maabara ya Sheria (Mtandao “X”).

#KonceptTvUpdatesImageProducer; Emma the Boy

Related Posts