Scholz amtabiria ushindi Harris katika uchaguzi wa Marekani – DW – 24.07.2024

Kansela Scholz amejitokeza mbele ya waandishi habari hii leo kujibu maswali kuhusu utendaji wa serikali yake, huu ukiwa mkutano wake wa tatu wa aina hii kabla ya kwenda mapumziko ya majira ya joto. Mkutano huo ambao uligeuka desturi ya kila mwaka chini ya mtangulizi wake Angela Merkel, unahusisha maswali kuhusu masuala mtambuka na maeneo yote ya kisera.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Scholz aliulizwa iwapo atafuata mfano wa Rais wa Marekani Joe Biden na kujiuzulu nafasi ya ukansela baada ya kumalizika kwa muhula wa sasa wa bunge, na baada ya kumshuru mwandishi alieuliza swali hilo alilolitaja kuwa zuri na la kirafiki, kansela huyo alijibu kwa kusema kuwa atawani tena. Scholz pia alisema anaamini inawezekana sana kwa Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris kushinda uchaguzi wa raisbaadae mwaka huu, inagwa alisitia kumuidhinisha waziwazi dhidi ya Mrepublican Donald Trump.

MSC 2022 - Kamala Harris na Olaf Scholz
Kamala Harris na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani mjini Munich katika mkutano wa UsalamacPicha: Sven Hoppe/REUTERS

Huyu ni mwanasiasa hodari na mzoefu ambaye anajua hasa anachofanya na ana mawazo yalio wazi kabisa kuhusu nafasi ya nchi yake, kuhusu maendeleo ya ulimwengu na kuhusu changamoto tunazokabiliana nazo. Na anayafanya haya kwa njia zake mwenyewe. Anajua anachotaka na anachoweza kufanya.”

Kuhusu ulinzi, Scholz amezungumzia azma ya serikali yake kupandisha matumizi ya kijeshi kufikia lengo la asilimia 2 ya pato jumla la taifa lililowekwa na Jumuiya ya Kujihami NATO, na kusema Berlin inanuwia kufikia lengo kupitia bajeti yake ya kawaidia baadae katika muongo huu. Scholz ametilia mkazo kwamba Urusi inahitaji kwanza kumaliza vita nchini Ukraine ikiwa inataka kuepusha uwekaji wa makombora ya masafa marefu ya Marekani nchini Ujerumani.

Soma: Makamu wa rais wa Marekani kufanya mazungumzo na viongozi wa Ulaya katika mkutano wa usalama wa Munich

Zaidi ya hayo, Kansela pia alizungumzia sula la uhamiaji haramu na kufukuwa kwa wahamiaji haramu na kukataliwa lwa waomba hifadhi, baada ya mahakama ya Ujeruman kukataa siku ya Jumatatu, madai ya hadhi ya kulindwa ya raia wa Syria alietiwa hatiani nchini Austria kwa kushiriki ulanguzi wa watu barani Ulaya.

Mahakama hiyo pia ilisema hakuna tena hatari jumla kwa raia wote kutoka mzozo wa muda mrefu wa Syria.Alipoulizwa kuhusu hukumu hiyo, Scholz alisema Ujerumani itaanza kuwarejesha wahalifu nchini Afghanistan na Syria, kama alivyotangaza mwezi uliopita.

Je Kamala anaweza kumshinda Trump katika uchaguzi 2024?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kuhusu vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza, Scholz amesisitiza haki ya Israel kujilinda huku akisisitiza uungaji mkono wa Ujerumani wa suluhisho la mataifa mawili. Pia ameihimiza israel kuheshimu sheria za kimataifa wakati akiendesha kampeni yake ya kijeshi dhidi ya Hamas.

Kampeni za Kamala: Harris afanya kampeni katika jimbo la Wisconsin

Scholz alionekana kuwa na matumaini kwamba chama chake kitapata uungwaji mkono zaidi katika uchaguzi mkuu ujao. Kura hiyo huenda ikafanyika Septemba 28, 2025, baada ya Baraza la Mawaziri la Ujerumani kukubali leo kupendekeza tarehe hiyo kwa Rais Frank-Walter Steinmeier.

 

Related Posts