Na Oscar Assenga,TANGA.
SHAURI la Maombi Madogo ya Jinai ambalo lilifunguliwa na Kombo Twaha Mbwana dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) na wenzake ambalo liliitwa Julai 23 mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga mbele ya Jaji Hapiness Ndesamburo kwa ajili ya kutolewa amri muhimu limesongezwa mbele mpaka Julai 26, 2024.
Katika Shauri hilo Kombo Twaha Mbwana aliwakilishwa na Mawakili wake Peter Madeleka na Wakili Solomon Kabondu ambalo lilisongezwa mbele kutokana na Jaji Hapiness Ndesamburo kutokuwepo.
Akizungumza mara baada ya kuhairishwa kwa shauri hilo na Naibu Msaijili wa Mahakama hiyo P R Nyaki, Wakili Peter Madeleka alisema kwamba kombo alikwenda mahakamani hapo kupitia mawakili wake ili kuiomba mahakama iwalazimishwe mamlaka au watu wanaomshikilia kinyume cha sheria impelekea mahakamani.
Alisema kwamba wao wanataka mahakamani ieleze kwanini imekuwa ikimshikilia muda wote huo na kwamba kama wanasema kombo ana makosa waje wamwambie wanafanya hivyo kwa mamlaka gani.
“Wanasema Kombo ana makosa waje wamuambie jaji sisi tupo tayari kuionyesha mahakama kwamba alichofanyiwa kombo ilikuwa sio haki na hakikuwa sahihi na ndio maana tumekuja kumwakilisha mteja wetu ambaye kwa takribani mwezi hajaonekana kwenye jamii na baadae ikataarifiwa kwamba Jeshi la Polisi lilimkamata na kumpelekea mahakamani kwa njia ambazo wao mawakili wake hawazijafahmu na sasa wanaambiwa amehifadhiwa kwenye gezara za maweni “Alisema Wakili Madeleka
Alisema kwamba walifungua shauri la maombi madogo ya jinai likiwa na lengo la kuitaka mahakama kuilazimisha mtu yoyote au mamlaka yoyote ya serikali inayomsikilia kombo kwa siku zote hizo kinyme na sheria waweze kuleta mahakamani na mahakama iweze kupata nafasi ya kujua kombo anahatia au hana na kama ameshikiliwa kinyume cha sheria basi iweze kutoa haki kwa mteja wao.
Aidha alisema kwamba kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji Mhe Hapines Ndesamburo walipewa wito ndio maana wamefika na wameambiwa jaji hayupo badala yake na wakaenda kwa ambapo shauri limehairishwa mpaka tarehe 26 Julai 2024.
Madeleka alitoa wito kwa wapenda haki wote kwamba maovu yanapotokea kwenye jamii na kukandamiza haki za watu wanapaswa kupingwa kwa nguvu zote na suala la kombo limezua mjadala mkubwa kwenye jamii na walitegemea hapo mahakamani ndio ilikuwa sehemu shtahiki ya mambo yote kuweza kujulikana na haki iweze kutendeka.
Alisema wao kama serikali wanaamini kombo alifanya makosa wanapaswa kushughulikia kwa mujibu wa taratibu za kisheria na sio vyenginev lakini ikitokea kunatokea mambo ya kupigiana pigiana simu mahakamani kukwepesha haki na kuchelewa haki wao hawatakubali watapambana mpaka hatua ya mwisho kuhakikisha kombo anapata haki yake.
“Natuma ujumbe kwa wale wote ambao wanasubiri mpaka kombo apone maana wameambiwa ni mgonjwa kwamba akishapona watamleta mahakamani ule udhalimu ambao wamemfanyia hautaonekana lakini kombo apone asipone afe asife sisi tutakwenda mahakamani kudai haki yake”Alisema Wakili huyo.
Wakili huyo alitoa wito kwa Jaji Mkuu kuhakikisha mahakama hazichezewi na watu wakikosa imani na mahakama wataamua kujichukulia sheria mkononi kombo ameamua kuwa mstaarabu kufungua kesi kupitia mawakili wake wanakuja mahakamani wanapewa udhuru Jaji hayupo.
“Ukisoma ibara ya 107 ibara ndogo ya pili ya katiba ya Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania inasema mahakama haipaswi kuchelewesha upatakaji wa haki kwa sababu zisizokuwa za msingi mahakama ailipanga kesi hiyo isikilizwe leo 23, Julai ilipaswa kujua kama kuna jambo la dharura basi kesi hiyo isingepaswa leo”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba aliyepanga ni mahakama na wanakwenda mahakamani na kuambiwa Jaji hayupo inaweza kuleta sura mbaya kwa jamii kwamna mahakama inashiriki kwenye kukwamisha haki za watu wanaamini kwamba tarehe 26 Julai waliopangiwa watakapokuja wanataka mahakama itimiza wajibu wake kwenye kutoa haki.
Akizungumzia sababu za Kombo kufungua kesi,wakili Madeleka alisema alifungua kesi hiyo kwa siku ambazo hakuonekana kwenye jamii kama kuna kesi nyengine wanadai wameshtaki nayo watakuja kuieleza mahakama maana wanataka waje wawaeleze wameshtaki kwa kosa gani na walimtoa wapi maana ikikumbukwe baada ya kombo kutokuonekana kwenye jamii familia ilienda kufungua kesi kwenye kitua cha polisi Handeni.
Alisema kwamba sasa polisi wanapoibuka kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ( RPC) kudai kwamba wanamshikilia Kombo na baadae wakampeleka mahakamani na hawajui ni mahakama gani wanapaswa kutueleza walimtoa wapi kwa sababu ndio hao hao polisi walirekodi taarifa zao za kwamba amepotea na anatafutwa na hawajawahi kutuambia amepatikana.
“Lakini pia alifanya kosa lipo maana kosa ambalo limeibuka baada ya kombo kupotea sasa taarifa za kupatikana kwake tuambiwa na taarifa za kupotea kwake na baadae tuambiwe kombo amefanya makosa ya kimtandao na sasa yupo magereza sasa awepo magereza asiwepo kapigwa hajapigwa tutakutana hapa mahakamani na wasione mahakama jamhuri waje wao sisi tupo kwa ajili ya kutetea haki za watu tunaamini kwa yale yaliyoyafanywa na wao tunataka waje watuambie wanachokifanya kwamba kombo anaapaswa kupewa haki”Alisema