SOKO LA MSAMVU LAUNGUA MOTO USIKU WA KUMKIA LEO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Zaidi ya vibanda tisa vya Wafanyabiashara vilivyopo pembezoni mwa stendi ya Msamvu Manispaa ya Morogoro vimeteketea kwa moto huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

 

 

Baadhi ya Wafanyabiashara katika stendi hiyo wamesema waliona moto unawaka katika moja ya kibanda ndipo ukazagaa katika maeneo mengine.

 

 

Mwakilishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Morogoro, Daniel Myala amesema hadi saaa hakuna madhara kwa Binadamu lakini mali zimeteketea na kwa sasa bado uchunguzi unaendelea Ili kufahamu chanzo cha moto huo.

 

Chanzo : Millard Ayo

Related Posts