VIJANA TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA – JOKATE – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amewasihi Vijana wote nchinikujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

 

“Viongozi wetu wanafanya kazi kubwa ya kutusemea katika mambo mengi makubwa, hivyo ili tuwape shime na nguvu lazima tujitokeze kwa wingi kwenda kuboresha Taarifa zetu kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura Ili wakati wa kupiga kura ukifika tukawapigie kura za kishindo”

 

 

Jokate aliyasema hayo Mkoani Kigoma alipoongoza Jogging maalum ya hamasa kwa Vijana kujitokeza kuboresha na kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga lililozinduliwa Mkoani hapo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa tarehe 20 Julai 2024

Related Posts